Translations: English – French – Portuguese – Spanish

Ni wakati wa mabadiliko​

Tunapongeza sasisho mliopendekeza katika mfumo wa kimataifa juu ya sifa za wahitimu, taaluma na umahiri wa wahandisi na kutambulika kuwa wahandisi wanahitaji kufuzu ili kukabiliana na changamoto za karne 21. Lakini kiungo muhimu kinakosekana ili kusuluhisha changamoto kuu za karne hii. Wahandisi lazima waweze kufikiria kwa makini jukumu la uhandisi wenyewe.

 

Mfumo wa Wahandisi Bila Mipaka ilianzishwa na lengo la kufanya uhandisi kuwezesha kuwa kwa mabadiliko, kuwa taaluma ya uhandisi utaleta mabadiliko yatakayowafanya watu na vitu vyenye uhai kuendelea kufanaya vyema kwenye sayari. Hapo awali ulianzishwa Ufaransa miaka ya 1980 ili kuangazia dhuluma kijamii, lakini sasa umesambazwa ulimwengu mzima. Lengo lake kuu likiwa kuwasaidia watu na sayari

 

Wengi wetu katika mfumo huu wamegundua kuwa elimu na kuendelea kwa wahandisi ni muhimu uhakikishwe kuwa unalenga uhandisi wote unalenga kuleta mguso kwa watu wote sasa na hata siku za usoni. Wasiwasi umeibuka kuwa elimu ya wahandisi haiwaandaa wahandisi vilivyo na tajriba zinazohitajika Ila kuleta mabadiliko, hasa vile matatizo ya kijamii na kimazingira yanavyozidi kuongezeka. Matukio ya 2020 yasiyotabirika, yakiongenezwa na mabadiliko ya hali ya anga yameongeza wasiwasi. Kuna uwezekano mwembamba wa kati ya miaka kumi ya kurekebisha hali, Ila Iwapo tutachelewa zaidi hatutaweza kuzuiza uharibifu. 

 

Pendekezo la kisasa lilorudiliwa na International Engineering Alliance’s Benchmark for Graduate Attributes and Professional Competencies limechukua hatua kubwa la kuzungumzia wasiwasi hizi.Ili kutambua hitaji la wahandisi kuhusisha shughuli zao kwenye malengo za kujikimu na kujiendeleza za UN, na kutambua uharibifu unaoweza tokea siku za usoni za kiteknologia, hayo marudio yanalenga kutambuliwa kwa jukumu ambazo wahandisi wanaweza na wanazohitaji Ili kugusia na kusuluhisha changamoto yanayokumba ulimwengu

 

Lakini mfumo wenyewe haukutambua hitaji la msingi la kubadilisha mawazo juu ya uhandisi: hitaji la wahandisi kufikiria kwa makini juu ya Uhandisi wenyewe. 

 

Katika marudio, uhandisi unaendelea kukuzwa kama mchakato usioshawishika na maadili kijamii Ili kusababisha suluhisho moja sahihi, ilhali ni mchakato tata uliiokitiri kwenye jamii na inahusisha mambo ya maadili muhimu na bila wasiwasi, kutoa hukumu bila uhakika na ujumbe wa kuchosha na kuzoea muktadha–na inalenga kuendeleza–mtazamo mwembamba wa uhandisi, usiyotambua kimaantiki kuwa uhandisi wenyewe una umuhimu na matokeo wanadamu na sayari. 

 

Kufikiria kwa makini swala la uhandisi inahusisha uwezo wa kuliona kama sehemu ya tatizo husika. Kama zoezi linalohusisha hali za ujenzi, utengenezaji na matumizi ya sitima, chakula na usambazaji wa maji, usafiri, mawasiliano na uchunguzi wa anga, na mengineyo uhandisi una umuhimu mkubwa katika maisha yetu ya kila siku na siku za usoni. Licha ya uhandisi kutusaidia katika burudani, afya na usalama, pia imetutia katika hatari zinazotawala ulimwengu wa leo.

 

Hali ya kuangazia umuhimu wa uhandisi unafanya swala la uhandisi kuwa muhimu sana katika kusuluhisha matatizo yaliyoko ulimwenguni ili tupate njia zetu katika changamoto zilizoko kwenye karne hii ya 21, kwa sababu umetambua ugumu na kujenga ujuzi wa kuiendeleza; kumeendeleza kufanywa kwa maamuzi ya kujitakia yanayozingira swala la uhandisi na pia imeonyesha umuhimu wa kuwahusisha wadau Ili kuja na suluhisho thabiti ikilinganishwa na kutengeneza vikao vya kuzuru na kujifunza 

 

Ili kuangazia malengo ya mfumo Shirika letu la Wahandisi Bila Mipaka linasema kuwa yafuatayo ni muhimu katika kuwabadili wahandisi waliosomea uhandisi wa karne 20 wawe na uwezo wa kuangazia changamoto za karne 21:

  • Kusisitizwa kwa kufikiria kwa makini kama msingi wa kujengea umahiriwa uhandisi, kuchunguza na kulinganisha kwa umakini jukumu la uhandisi, uhusiano wake kwa wanadamu na umuhimu wake katika maisha yetu ya hapo awali na yajayo

  • Ufahamu wa mambo ya maadili yenye asili ya uhandisi juu ya uhusiano wa uhandisi, wanadamu na sayari na kusisitiza umuhimu wa kukuza ujuzi unaohitajika kukumbana na utata wa mambo ya kihandisi.

  • Elimu inayohitajika kutoa hukumu muhimu wa kihandisi itambuliwe kwa upana, Ikijumuishwa na kutambua umuhimu wa masomo ya sayansi katika kuwasaidia wahandisi kuelewa maana ya kazi zao.

Shirika letu la Wahandisi Bila Mipaka inasaidia wanafuzi na waliofuzu kukuza taaluma za kuangazia na kufikiria kwa makini swala la uhandisi, na kwa kujenga mahusiano wanasayansii wa kijamii, viongoziasili, na makundi mengine yaliyo na uhusiano na uhandisi na jamii. Tungekaribisha fursa ya kufanya kazi kwa karibu na International Engineering Alliance na mashirika mengine yatakayo piga jeki swala la uhandisi

 

Hatuna sayari B na muda unazidi kuyoyoma. Ili kuhakikisha uhandisi unawafaidi wote, mawazo ya wahandisi lazima yaelekezwe katika kuwaza na kufikiria kwa makini juhudi la uhandisi wenyewe.

 

Matamshi haya yametungwa na Wahandisi wa Kimataifa Bila Mipaka na uthibitisho maalumu ufuatao wa Shirika la Wahandisi Bila Mipaka (yameasilishwa kulingana na herufi ya kuanza): Australia, Brazil, India, Kanada, Marekani, Uholanzi, Ufilipino, Uingereza.

 

Wahandis wa kimataifa Bila Mipakak ina wawakilishi katika zaidi ya mataifa 60-100 ulimwengu mzima na maelfu ya watu wanaounga mkono ndani ya sekta ya uhandisi na vyuo vya uhandisi.

 

Kwa maelezo zaidi, wasiliana nasi kupitia: admin@ewb-international.org.